#CAFWomensChampionsLeague: “Mimi kama mlezi wa timu ya JKT Queens, sina wasiwasi na vijana”

#CAFWomensChampionsLeague: “Mimi kama mlezi wa timu ya JKT Queens, sina wasiwasi na vijana”
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewatoa hofu Watanzania, akiwataka kuwa na imani na JKT Queens ambayo itaiwakilisha nchi na ukanda wa CECAFA kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake.

Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo leo baada ya kushuhudia droo ya kupanga makundi ambapo JKT Queens imepangwa kundi ‘B’ ikiwa pamoja na Gaborone United kutoka Botswana, Asec Mimosas kutoka Ivory Coast na TP Mazembe kutoka DR Congo.

#CAFWomensChampionsLeague

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *