Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka …Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka …

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, kampuni ya Smartpika kupitia Mradi wa Huduma za Kisasa za Upikaji (MECS) imegawa majiko sanifu ya umeme katika Shule ya Msingi Kibasila jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia nyumba milioni tano nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Smartpika, Andron Mendes, amesema mpango huo unalenga kuwafikia Watanzania milioni 20 ifikapo mwaka 2034, kwa lengo la kuwawezesha kutumia nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu.

Naye Mwakilishi wa Mpango wa MECS ulio chini ya Serikali ya Uingereza Charles Barnabas ambao ndio wanadhamini wa mpango wa huduma za kisasa za kupikia (MECS) amebainisha kuwa matumizi ya majiko sanifu ya umeme ni nafuu zaidi na yanachangia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Mpango wa MECS wa kukuza na kusaidia nishati ya umeme unaofadhiliwa na UK Aid ambao unatekelezwa Nchini Tanzaniua una lengo la kuharakisha mabadiliko ya matumizi ya kuni na mkaa kwenda kwenye matumizi ya umeme kwa shughuli za kupikia

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *