Katibu wa Itikadi, Siasa, Mafunzo na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga, Kipanga Salim, amewataka wakazi wa Jij…Katibu wa Itikadi, Siasa, Mafunzo na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga, Kipanga Salim, amewataka wakazi wa Jij…

Katibu wa Itikadi, Siasa, Mafunzo na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga, Kipanga Salim, amewataka wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, akisisitiza umuhimu wa kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga, Kipanga amesema chama hicho kimefanikiwa kuwafikia wanachama na wananchi katika maeneo mbalimbali kupitia mikutano ya hadhara, kampeni za nyumba kwa nyumba na majukwaa ya kisiasa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kunadi sera na ilani ya CCM kwa wananchi.

Amesema kuwa kampeni hizo zimekuwa zikitekelezwa kwa kuzingatia maadili ya kisiasa, huku akiwataka wananchi kupuuza maneno ya uchochezi na badala yake kujikita katika kufanya maamuzi yenye tija kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.

Kipanga aliongeza kuwa CCM itaendelea kuwa karibu na wananchi hata baada ya uchaguzi, kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ushirikishwaji wa vijana na wanawake katika shughuli za kisiasa na kiuchumi, sambamba na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama na jamii kwa ujumla.
#startvupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *