Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanaongoza mbio za kumsaka mshambuliaji wa Marseille Muingereza Mason Greenwood, ingawa Tottenham na West Ham pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (TeamTalks)
Manchester United na Newcastle wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Uingereza Elliot Anderson, huku Nottingham Forest wakidai ada ya kati ya £100m na £120m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Florian Plettenberg).
Jobe Bellingham hana nia ya kujiunga na Manchester United, ambayo imekuwa ikifikiria uwezekano wa kumnunua kiungo huyo wa kati wa Borussia Dortmund Muingereza mwenye umri wa miaka 20. {Mirror)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United itazuia maombi ya uhamisho kutoka kwa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, na mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, ikiwa wataomba kuondoka Januari. (The Sun)
Manchester United imewapa Napoli mwanga wa kijani kutekeleza wajibu wao wa kumnunua mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, mwezi Januari. (Mirror),
West Ham wamemfanya mlinzi wa Lille na Brazil Alexsandro kuwa kipaumbele chao katika dirisha la uhamisho la Januari, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa na thamani ya £26m. (ESPN Mexico – In Portuguese)
Chanzo cha picha, Getty Images
Vinicius Jr, 25, “anafikiria kwa uzito” matarajio ya kuondoka Real Madrid baada ya kusema kusikitishwa kwake na meneja Xabi Alonso, ambaye alimbadilisha fowadi huyo wa Brazil mwishoni mwa mechi ya Jumapili ya El Clasico. (AS – In Spanish)
Juventus wameanza mazungumzo na mkufunzi wa zamani wa Napoli na Italia Luciano Spalletti, 66, kuhusu kuwa kocha wao mkuu baada ya kumfukuza Igor Tudor. (Gianluca di Marzio – In Itali)
Tottenham, Arsenal na Newcastle wanamfuatilia mshambuliaji wa Porto na Uhispania Samu Aghehowa, 21. (Fichajes – In Spanish)