Chanzo cha picha, TANZANIA
Huduma za kivuko kati ya mji wa kibiashara wa Tanzania wa
Dar es Salaam na Zanzibar zitasimamishwa Oktoba 29, 2025, wakati nchi hiyo
itakapokuwa na uchaguzi mkuu.
Waendeshaji pekee, Azam Marine na Zan Fast Ferries
wametangaza kuwa hakuna feri zitakazoendesha shughuli zake katika mwelekeo
wowote hadi Oktoba 30.
Katika taarifa tofauti, makampuni hayo mawili yamesema
uamuzi wa kusimamisha huduma hizo ulifanywa ili kuwezesha ushiriki wa wapiga
kura katika uchaguzi.
Vivuko vinavyoendeshwa na wawili hao, husafirisha karibu
abiria 10,000 kila siku kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.
Mabrouk Hussein, msafiri wa kawaida kati ya maeneo hayo
mawili, aliiambia BBC, “Nashangaa. Kwa nini iwe hivyo? Itakuwaje ikiwa mtu
anahitaji kusafiri kwa ajili ya mazishi au matibabu?
Hii si haki, inaonekana ina madhumuni ya kisiasa. Kwa nini
sasa? Sio kila mtu anapenda kupiga kura.
Baadhi ya
mabasi kusimamisha huduma
Baadhi ya makampuni ya mabasi ya umbali mrefu pia
yametangaza kuwa huduma za kwenda na kutoka Dar es Salaam zitasitishwa.
Siku ya uchaguzi, baadhi ya mabasi hayataendesha hadi miji
mikubwa kama Mwanza, Tarime, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Bukoba na Kigoma.
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimesema
kusimamishwa kwa shughuli za usafiri kunalenga kuwawezesha wafanyakazi wa
usafirishaji na abiria kupiga kura zao.
Hata hivyo, Shirika la Haki za Abiria limekosoa uamuzi huo
na kudai kuwa shirika la wamiliki limeshindwa kuzingatia wajibu wa kijamii na
familia.
Pia unaweza kusoma: