
Baraza la Haki za bindamu la Umoja wa Mataifa, limewateua watalaam watatu, kuchunguza madai ya ukiukwaji wa haki Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia uhaba wa bajeti ya fedha, kuwaisaidia watu wanaoishi kwenye changamoto za kibinadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tume hiyo, imeteua Arnauld Akodjenou kutoka Benin, kuongoza watalaam hao kuchunguza hali ya haki za binadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini.
Wengine ni pamoja na Maxine Marcus mtalaam wa masuala ya haki za biandamu kutoka Ujerumani na Clement Nyaletsossi Voule kutoka Togo.
Tangu waasi wa M 23 walipoteka miji ya Goma na Bukavu mapema mwaka huu, Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya watu wamesalia wakimbizi.
Kazi ya watalaam hao itakuwa ni kuchunguza kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC, kubaini hasa kinachotokea, wanaohusika na ukiukwaji wa sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Mapema mwezi huu, Baraza hilo la Umoja wa Mataifa, lilitaka ufadhili wa uchunguzi huo, ambao sasa utafanyika kuanzia mwezi Januari 2026 na ripoti ya kwanza kuwekwa wazi mapema mwaka 2027.