Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema lawama, manung’uniko na matusi mitandaoni, hayaamui kuhusu mwelekeo wa nchi, kinachoamua ni kwenda kupiga kura.
Kutokana na uhalisia huo, amewataka wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kesho Oktoba 29, kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi, kama walivyohudhuria kwa wingi kwenye mikutano ya kampeni.
Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Oktoba 28, 2025 alipowahutubia katika mkutano wa kuhitimisha kampeni zake za urais, uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
“Si vyema kubaki kujadili na kulalamika mitandaoni, wanaofanya maamuzi ya mwelekeo wa nchi yetu ni wale wanaopiga kura, sio wale wanaolalamika.
“Lawama, kebehi na matusi havichagui wala kubadilisha viongozi, kura huchagua na kukataa viongozi wazembe, twendeni kwa wingi wetu tukapige kura,” amesema mgombea huyo.
#StarTvUpdate
