Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa mpango wa d…Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa mpango wa d…

Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa mpango wa dharura uliaoanzishwa chini ya TANROADS kufuatia maafa ya mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua za El Nino na Kimbunga Hidaya kuanzia mwezi Oktoba 2023 hadi Mei 2024.

Mradi unatekelezwa chini ya miradi mikubwa inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, ikiwemo TanTIP, RISE, MBDP na dirisha la CRW huku lengo kuu la mradi ikiwa ni kurejesha mawasiliano ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa, ili wananchi waendelee kupata huduma muhimu na shughuli za kiuchumi ziendelee bila usumbufu.

Akizungumzia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huu, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania-TANROADS Mhandisi Mohamed Besta amesema kuwa Ujenzi wa miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya dharura inayotekelezwa katika mikoa 22 ya Tanzania Bara ikihusisha miradi 81 ya dharura ambayo inahusisha ujenzi na ukarabati wa madaraja, barabara, mitaro na makaravati yaliyoharibiwa.

Amesema kuwa jumla ya fedha zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ufadhili wa Benki ya Dunia ni Dola za Marekani milioni 325 (sawa na takribani Shilingi bilioni 840) ambazo zinatekeleza miradi hiyo chini ya mpango wa CERC (Contingency Emergency Response Component), ambapo inatekelezwa na makampuni ya wakandarasi wazawa 70 na makampuni 11 kutoka nje ya nchi.

Mhandisi Besta amesema kwa sasa, maendeleo ya utekelezaji yapo katika wastani wa asilimia 68 ambapo miradi 12 imekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 hadi 100, na miradi mingine 53 ipo kati ya asilimia 50–95 ya utekelezaji.

#SyarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *