
Kupunguzwa kwa misaada katika nchi za Afŕika Mashariki kumesababisha kesi za watoto kuzaliwa na Virusi vya Ukimwi kwasababu akina mama hawakuweza kupata dawa, kuongezeka kwa magonjwa hatarishi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na ripoti ya madaktari wa Haki za Binadamu, angalau mwanamke mmoja alitoa mimba kwa kukosa usaidizi, madaktari hao wakihusisha haya na kukatizwa kwa utaratibu wa Pepfar – mpango wa dharura wa marais wa misaada ya UKIMWI kwenye nchi za Tanzania na Uganda.
Programu ya Pepfar, iliyokuwa inaratibiwa na Marekani, ilianzishwa mwaka 2003 na ina sifa ya kuokoa mamilioni ya maisha, hasa katika mataifa ya Afrika yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Wahudumu wa afya waliripoti uhaba wa dawa za kudhibiti virusi hivyo na kusababisha ongezeko la maambukizi kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na watoto kuzaliwa na virusi hivyo kwa sababu akina mama hawakuweza kupata dawa za kuzuia maambukizi.
Nchini Tanzania na Uganda, programu za kuzuia na matibabu ya VVU zilitegemea mpango wa Pepfar na agizo la kusimamisha kazi zake ilimaanisha kuwa kliniki hazikuweza kutoa dawa zilizonunuliwa kwa pesa za Marekani kwa siku kadhaa.