ECOWAS, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, inathibitisha kuwa imetuma ujumbe wa kiufundi nchini Sierra Leone kutathmini mzozo wa mpaka na Guinea karibu na kijiji cha Yenga. Eneo hili la mashariki mwa nchi hiyo limekaliwa kwa mabavu na jeshi la Guinea tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone, vilivyomalizika mwaka 2002, licha ya makubaliano kadhaa ya kurejesha sehemu hiyo ardhi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na afisa kutoka shirika la kikanda la ECOWAS, hii ni misheni ya tathmini, inayojumuisha mafundi waliopewa jukumu la kuelewa hali na kuripoti. “Hawana uwezo wa kufanya maamuzi,” ECOWAS inaeleza. Ripoti yao itawasilishwa kwa wakuu wa nchi za Guinea na Sierra Leone, kwa mujibu wa pendekezo la mkutano uliopita wa ECOWAS.

Mnamo Agosti 29, wajumbe hao walisafiri hadi Koindu, Sierra Leone, mji wa mpakani karibu na Yenga, ili kuona hali hiyo pamoja na watawala wa eneo hilo. Lakini siku iliyofuata, mvutano uliongezeka, anasema Mbunge wa Sierra Leone kutoka eneo la Yenga, Fallah Kenawah Tengbeh.

“Mnamo Agosti 30, saa 8 usiku, vikosi vya Guinea vilifyatua risasi hewani. Siku iliyofuata, wanajeshi waliokuwa na silaha waliingia katika ngome za wanajeshi wa Sierra Leone kabla ya kuondoka. Huu ni uchochezi. Watu wetu wanateseka, bila chakula, huduma za afya, au elimu. Hatujaridhishwa hata kidogo na mtazamo wa vikosi vya usalama vya Guinea.”

ECOWAS itakutana na mamlaka ya Guinea kabla ya kukamilisha ripoti yake. Lakini kwa Mbunge Tengbeh, anasema kuingilia kati moja kwa moja kwa Julius Maada Bio, Rais wa Sierra Leone na rais wa sasa wa ECOWAS tangu mwezi Juni, hatimaye kunatoa msukumo kwa suala hili linalodumu miaka ishirini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *