.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 28, kutoka Napoli. (TeamTalks)

Napoli itafanya jaribio lingine la kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 20 kutoka Manchester United mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport – In Italy)

Kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 28, ana nia ya kuondoka West Ham mwezi Januari. (Times – Subscription Required).

Manchester City wameanza mazungumzo na kiungo wa kati wa safu ya ulinzi wa Uhispania Rodri, 29, kuhusu kandarasi mpya na wana uhakika wa kufikia makubaliano mwishoni mwa mwaka huu. (TBR Football,)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham hawana uwezekano wa kumsajili Marc-Andre ter Stegen kutoka Barcelona mwezi Januari, lakini uhamisho wa mkopo kwenda Chelsea unaweza kuwezekana kwa mlinda lango huyo wa Ujerumani, 33. (Teamtalk)

Chelsea na Tottenham zilionyesha nia ya kutaka kumnunua Morgan Rogers, 23, wakati wa majira ya joto lakini Aston Villa kwa sasa wanafanya mazungumzo na kiungo huyo wa kati wa Uingereza kuhusu mkataba mpya. (Fabrizio Romano,)

Fabio Carvalho ataondoka Brentford mwezi Januari, huku uhamisho wa kudumu ukizingatiwa kwa winga huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23. (Florian Plettenberg), nje

Sunderland wanapanga mpango mwingine wa kumnunua Marc Guiu kwa mkopo mwezi Januari baada ya Chelsea kumrejesha nyumbani mshambuliaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 katika mechi mbili tu za uhamisho wa mkopo walizokubali msimu uliopita. (Football Transfrers)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wanatazamia kujiimarisha katika nafasi ya beki wa kulia kwa kumuongeza mchezaji wa Strasbourg Guela Doue, ingawa Aston Villa na Brighton pia wako kwenye kinyang’anyiro cha kumnasa mlinzi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 23. (Football Transfers)

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyofikiria kumnunua Joel Ordonez wa Club Brugge, huku Newcastle na Aston Villa pia wakiwa kwenye mbio za kumsajili beki huyo wa kati wa Ecuador, 21. (Ekrem Konur)

Manchester United wako kwenye mazungumzo juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa AIK mwenye umri wa miaka 16 kutoka Sweden Kevin Filling. (Florian Plettenberg)

Robbie Keane, Kieran McKenna na Ange Postecoglou wote wako kwenye orodha fupi ya kumrithi Brendan Rodgers kama meneja wa kudumu wa Celtic. (Telegraph – Subscription Required)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *