Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wako tayari kumwachia kipa wa Cameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29, ajiunge na timu ya Saudi Arabia kwani dirisha la usajili kwa ligi hiyo bado liko wazi. (Teamtalk)
Kiungo wa Brazil, Casemiro (33), aliamua kubaki Old Trafford badala ya kwenda Al-Nassr ili kuongeza nafasi yake ya kucheza Kombe la Dunia 2026. (Goal)
Aliyekuwa kocha wa Tottenham, Ange Postecoglou, anatajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaofikiriwa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag huko Bayer Leverkusen baada ya Hag kutimuliwa kazi wiki hii (Sky Sports Germany)
Klabu ya Uturuki, Fenerbahce, iliyomtimua Jose Mourinho hivi karibuni, pia inaweza kuwa chaguo lingine la Postecoglou (60), ambaye aliipa Spurs ubingwa wa Europa League msimu uliopita kabla ya kutimuliwa. (Fabrizio Romano)
Arsenal walikuwa tayari kumuuza winga wa Brazil Gabriel Martinelli (24) mwanzoni mwa dirisha la kiangazi, lakini dau lao la £60m liliwatisha klabu zilizokuwa tayari kutoa si zaidi ya £40m. (Mail)
Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Brazil, Antony (25), amesema alizungumza na Bayern Munich kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United kwenda Real Betis, klabu aliyowahi kuichezea kwa mkopo msimu uliopita. (El Partidazo, via Mirror)
Klabu ya Juventus ilijaribu kwa muda mrefu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani (26) kutoka Paris Saint-Germain, lakini Tottenham wakafanikiwa kumbeba. (Gazzetta dello Sport)
Manchester United bado wanavutiwa na kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo, lakini mkurugenzi wa soka Jason Wilcox haoni kama ndiyo kipaumbele cha kwanza kwa sasa. (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal na Barcelona wanamfuatilia kwa karibu beki wa Nottingham Forest, Murillo (23), raia wa Brazil. (Caughtoffside)
Nyota wa Nottingham Forest, Jota Silva (26), bado anaweza kuondoka kwenda Saudi Arabia au Uturuki baada ya mpango wa dakika za mwisho kujiunga na Sporting kuvunjika. Klabu ya Neom SC kutoka Saudi inamtaka. (Talksport)
Forest wanataka kukusanya fedha kwa kuuza baadhi ya wachezaji baada ya msimu wa kiangazi kununua wachezaji wapya 13 kwa kikosi cha kwanza. (The Athletic)
Aliyekuwa kocha wa Wolves, Gary O’Neil, amesema hana haraka kurudi kwenye kufundusha na anasubiri nafasi sahihi, na wakati sahihi licha ya kuzungumza na vilabu vikubwa kadhaa. (Telegraph)