Wakati nchi nyingi zikijiandaa kulitambua Taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu ujao wa Umoja wa Mataifa, Israel inatishia kujibu kwa kunyakua maeneo yanayokaliwa kwa mabavu. Leo Alhamisi, Septemba 4, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anatarajia kuongoza mkutano wa ngazi ya juu ambapo watachunguza uwezekano wa kutumia “uhuru wa Israel” kwa baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi. Huu ni mpango wa kuunganisha kwa Israel maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1967.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Frédérique Misslin

Kwa siku kadhaa, suala hili limekuwa mada kuu katika kwenye vyombo vya habari vya Israel: swali sio ikiwa kutakuwa unyakuzi wa maeneo ya Palestina, lakini ukubwa wake utakuwa wa aina gani. Chaguzi kadhaa zimejadiliwa wakati wa mikutano ya serikali ya hivi punde zaidi: unyakuzi wa nguvu kwa baadhi ya kambi za makazi zilizounganishwa katika Bonde la Yordani. Pia kuna uwezekano mpana wa kunyakuliwa kwa eneo C, ambalo linawakilisha 60% ya eneo la Wapalestina. Eneo C ni eneo ambalo kwa sasa liko chini ya udhibiti kamili wa Israel kwa usalama na utawala.

Bezalel Smotrich anaenda mbali zaidi

Waziri wa Fedha wa Israel kutoka mrengo mkali wa kulia Bezalel Smotrich anataka kwenda mbali zaidi na kuzungumzia unyakuzi, akidai “kutumia” mamlaka ya Israel juu ya 82% ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ambapo Wapalestina milioni tatu na walowezi 700,000 wa Israel, wanaochukuliwa kuwa haramu chini ya sheria za kimataifa, wanaishi hivi sasa. Katika mpango wake, Smotrich anaacha miji sita mikubwa, ikiwa ni pamoja na Nablus na Ramallah, kwa Wapalestina.

Majadiliano haya yanakuja wakati kanuni ya mpango wa makazi katika eneo E1 ilikuwa tayari imeidhinishwa msimu huu wa kiangazi wa mwaka 2025. yanatoa ujenzi wa nyumba 3,400 ambazo zingezuia mwendelezo wowote wa kijiografia kati ya kaskazini na kusini mwa Ukingo wa Magharibi.

Kwa upande wake, Falme za Kiarabu, ambazo zilifufua uhusiano na Israel mwaka 2020, zilionya mnamo Septemba 3 dhidi ya jaribio lolote la Israel la kunyakua maeneo ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambapo zinauelezea kama “mstari mwekundu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *