Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar ZEC imemtangaza Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa nddiye mshindi wa uchaguzi wa urais baada ya kupata zaidi ya asilimia 74 ya kura, katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 29.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jaji George Joseph Kazi, amesema Rais Hussein Ali Mwinyi, ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 74.8 ya kura akifanikiwa kutetea kiti chake kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, , akimshinda mpinzani wake wa karibu Othman Masoud Othman wa Chama cha ACT-Wazalendo, aliyepata asilimia 23.2 ya kura.

Kufutia ushindi huo Rais Minyi ataendelea kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka kama Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwaka wa 2030.

Zoezi la upigaji kura visiwani Zanzibar lilianza Oktoba 28 kwa kile kilichoitwa “kura ya mapema”, ikihusisha makundi maalumu, wakiwamo maafisa wa ulinzi na usalama na wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), waliokuwa kazini siku ya Uchaguzi Mkuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *