
Shirika la utangazaji nchini Tanzania, TBC, limeripoti kuwa rais mteule Samia Suluhu Hassan, ataapishwa hivi leo mjini Dodoma, siku chache kupita tangu atangazwe mshindi wa uchaguzi wa Octoba 29.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa shirika hilo, rais Samia ataapishwa katika uwanja wa kijeshi ambapo rai awa kawaida hawataruhusiwa kushuhudia tukio hilo.
Mwishoni wa juma lililopita, tume huru ya taifa ya uchaguzi, ilimtangaza Rais Samia kupata ushindi wa asilimia 97.66 ya kura zote, matpkeo ambayo yalitangazwa huku nchi hiyo ikishuhudia vurugu za uchaguzi katika baadhi ya miji.
Vurugu kwenye miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Songwe, zilianza tangu siku ya upigaji kura, ambapo baadhi ya raia walijitokeza barabarani kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo, wakishinikiza mabadiliko ya sheria za uchaguzi.
Licha ya Serikali kutotoa idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha au kujeruhiwa hadi sasa, mashirika ya kiraia nchini humo Pamoja na yale ya kimataifa, yanadai watu zaidi ya 700 walipoteza Maisha na mamia wengine kujeruhiwa idadi ambayo imekanushwa vikali na Wizara ya mambo ya nje.
Haya yanajiri wakati huu nchi hiyo ikiwa katika makataa ya watu kutembea usiku, wakati huu wanahabari wetu walioko nchini Tanzania wakiripoti kuanza kurejea kwa hali ya utulivu kwenye miji iliyoripotiwa vurugu, huku pia raia wakilalamikia kuhusu uhaba wa bidhaa za chakula na zilizoko kupanda bei maradufu.