Waangalizi wa uchaguzi toka Jumuiya ya SADC, wamesema raia wa Tanzania hawakuweza kuonesha maamuzi ya yao ya kidemokrasia katika uchaguzi wa juma lililopita kutokana na kile ujumbe huo umesema kuwepo kwa vitisho, udhibiti wa taarifa na kukosekana kwa upinzani thabiti.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti yah ii ya awali ya SADC imetolewa wakati huu kukiwa na taarifa mkanganyiko kuhusu idadi kamili ya watu waliopoteza Maisha kufuatia vurugu zilizoshuhudiwa siku ya upigaji kura na siku zilizofuatia.
Mkuu wa waangalizi wa SADC, Richard Msowoya, amesema kuwa walibaini katika baadhi ya maeneo ya nchi, wapiga kura hawakuwa huru.

Licha ya ujumbe huu kueleza kuwa kulikuwa na mazingira ya uwazi hasa katika hatua za awali za maandalizi ya uchaguzi wenyewe, kamepni kwa sehemu kubwa zilitawaliwa na chama tawala, huku vyombo vya Habari vya um ana binafsi vikionekana kutoa nafasi kubwa kwa chama tawala.
Aidha waangalizi hao wamesema kukosekana kwa wapinzani wakuu, akiwemo Tundu Lissu anayeendelea kusota rumande kwa tuhuma za uhaini Pamoja na kuzuiwa katika mazingira ya kutatanisha kwa mgombea wa chama kingine cha upinzani ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, ni wazi hakukuwa na usawa.

SADC pia ilitoa mapendekezo kadhaa kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru, haki na kuaminika, maoni ambayo wakatik wa hotuba yake yake, rais Samia alisema wanayapokea lakini wanakataa maagizo ya nini cha kufanya.
Rais Samia alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 98 ya kura zote, amtokeo ambayo yamekataliwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo, Chadema.