Pia aliwaombea wahanga wa maporomoko ya ardhi ya hivi majuzi na kuongeza kuwa kuenea kwa kipindupindu kunatishia maisha ya maelfu ya watu ambao “tayari wamechoka.”

Zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika kijiji kimoja cha Jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, kundi lenye silaha lilisema.

Kundi linalodhibiti eneo hilo, lilisema katika taarifa kwamba wakazi wote wa kijiji cha Tarsin kwenye Milima ya Marra waliuawa Agosti 31, baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maporomoko hayo.

Maafa hayo ya asili yalikuja huku kukiwa na mapigano makali kati ya jeshi na RSF, ambayo yameua zaidi ya watu 20,000 na wengine milioni 14 kuyahama makazi yao tangu Aprili 2023, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za mitaa. Utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani, hata hivyo, unakadiria idadi ya vifo kuwa karibu 130,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *