Eneo la Nyala la Sudan ndiko kulikofanyika sherehe Agosti 31 ambayo itabadilisha muelekeo wa taifa lililokumbwa na mapigano, yaliyochochewa na mfarakano wa kisiasa kuwahi kutokeo tangu kujiondoa kwa Sudan Kusini.

Mohamed Hamdan Dagalo, kiongozi wa wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la Sudan (SAF) linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan tangu Aprili 2023, alikula kiapo siku hiyo kama mkuu wa serikali pinzani.

Kiongozi wa wapiganaji Abdelaziz Adam al-Hilu, aliapishwa kama naibu wa Dagalo, na baraza la watu 13 linakamilisha utawala huo, kulingana na taarifa kutoka kwa muungano huo mpya wa Sudan.

Wakati wa kuundwa kwa serikali hiyo unaonekana kupangwa mahsusi kwenda sanjari na hafla iliyokuwa inaendelea kwa upande wa wapinzani wao. Siku chahe kabla, serikali inayoongozwa na al-Burhan, ilifanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri mjini Khartoum tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sasa, kukiwa na serikali mbili pinzani, wataalamu wanaona mgawanyiko wa taifa la tatu lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kusambaratika. Kuundwa kwa serikali pinzani, ambayo baraza la kijeshi limeitaja kuwa “serikali bandia”, pia inaonesha kuwa hakuna upande ambao unakaribia kupata ushindi.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wote wamekataa mamlaka ya serikali pinzani nchini Sudan, wakiitaja kama hatari kwa umoja wa nchi na uhuru wake.

Kupigania utawala

Mapigano ya kijeshi yako dhahiri katika eneo la El-Fasher, ambalo limekabiliwa na vita vya kijeshi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Picha za satelaiti kutoka Maabara ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Yale zinaonesha namna RSF ilivyoweka vizuizi kwa zaidi ya kilomita 31, vilivyozunguka mji na kufungia watu katika sehemu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *