Nchini Uganda, ripoti ya serikali inaonesha kuwa thuluthi moja ya watumishi wa umma, walitoa rushwa ya fedha ili kupata kazi walizonazo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkaguzi mkuu wa serikali katika ripoti yake, amebainisha kuwa asilimia 35 ya watumishi wa umma waliopata kazi kati ya mwaka 2018 hadi 2022, walilipia fedha kabla ya kupata nafasi hizo.

Idadi kubwa ya ajira zilizopatikana kwa namna hiyo ni katika sekta ya elimu na afya, katika nchi hiyo ambayo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya rushwa kwenye idara za serikali.

Aidha, ripoti hiyo inasema asilimia 25 ya watu walioajiriwa kwenye Wizara na idara mbalimbali za serikali, walitoa rushwa, ambapo watu walilipa kati ya Dola 500 hadi Elfu tano, ili kupata nafasi hizo.

Kati ya mwaka 2018 hadi 2022, raia wa Uganda waliotafuta ajira za serikali, walilipa karibu Shilingi Bilioni 29 za Uganda ili kuajiriwa.

Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa karibu miaka 40 sasa amekuwa akikiri serikali kukabiliwa na kiwango kikubwa cha ufisadi na kuahidi kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *