
Ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ule wa waasi wa AFC/M23, umekuwa jijini Doha kwa wiki tatu sasa kwa ajili ya mazungumzo ya amani, lakini hatua kubwa haijapigwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti kutoka kwenye mazungumzo hayo, zinasema, mpaka sasa hakuna mazungumzo muhimu yaliyofanyika.
Mpaka sasa pande zote, zimekwama kwenye kujengeana kuaminiana, hasa kuhusu suala tata la kuachiwa kwa wafungwa, jambo ambalo limeendelea kuwa kikwazo kwenye mazungumzo hayo.
Suala la kwanza, linaloonekana kukwamisha mazungumzo hayo kutopiga hatua lakini namna ya kuwaachia huru mamia ya wafungwa, linasalia suala kubwa ambalo halijapata ufumbuzi.
Waasi wa M 23/AFC wanasema serikali ya Kinshasa imewakamata watu zaidi ya 700, wakati huu Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, likiombwa kusaidia kuhakiki idadi hiyo.
Waziri wa usalama wa ndani Jacquemain Shabani, amesisitiza kuwa taratibu zitafuatwa kuhusu namna ya kuwaachia na kuwahakiki wafungwa hao, ambao wamezuiwa kwenye kambi za jeshi.
Serikali ya DRC, kati ya mwezi Januari na Februari, imewashtumu waasi wa M23/AFC kwa kuwazuiwa wanajeshi 1500 kwenye kambi ya kijeshi ya Rumangabo kwa ajili ya kuwageuza kuwa wapiganaji wake huku wengine zaidi ya 300 wakikamatwa.