ENGLAND: Manchester City watakuwa uwanja wa nyumbani wa Etihad kuwakaribisha Liverpool, mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa saa 1:30 usiku wa leo.
City wanaingia katika mchezo huo wakiwa nafasi ya tatu na pointi 19, na Liverpool nafasi ya sita pointi 18.
Mchezo uliopita City walishinda dhidi ya Bournemouth mabao 3-1, pia Liverpool walishinda mabao 2-0 dhidi ya Aston Villa.
Baada ya michezo ya wiki hii ya ligi mbalimbali, zitasimama kupisha mechi za FIFA za kirafiki, ambapo ligi zitarejea Novemba 21.
