SHIRIKA la Utafiti na Maendeleo ya Viwwanda Tanzania (TIRDO) pamoja Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yameingia makubaliano ya awali (MOU),kuhusu utafiti na uendelezaji wa Madini ya kimkakati (strategic minerals) yenye umuhimu mkubwa kwa usalama wa taifa, maendeleo ya viwanda, teknolojia ya kisasa, na uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO ,Profesa Mkumbukwa Mtambo amesema hayo wakati wa utiaji saini hati ya makubaliano ya awali kati Shirika lake na Stamico katika halfa iliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro.
Profesa Mtambo amesema madini hayo ni muhimu kwa sababu hupatikana kwa wingi mdogo duniani, ni vigumu kuyachukua au kuyabadilishiwa, na yanahitajika kwa teknolojia muhimu kama nishati safi, magari ya umeme, vifaa vya elektroniki, silaha, na ujenzi wa miundombinu.
Ametaja baadhi ya aina ya kuu za madini ya kimkakati ni Madini ya nishati safi (Clean energy minerals) ambayo hutumika katika teknolojia za nishati mbadala na magari ya umeme.
Profesa Matambo ameeleza baadhi madini hayo na matumizi yake katika mabano ni Lithium ( betri za magari ya umeme), Cobalt (betri na vifaa vya elektroniki).

Mengine ni Nickel (betri na chuma cha pua),Graphite (katodi za betri),Manganese (uzalishaji wa chuma na betri) na Madini adimu ya dunia (Rare Earth Elements – REEs) ambayo hutumika katika teknolojia za kisasa, mawasiliano, ulinzi na nishati.
Profesa Mtambo ametaja umuhimu wa mradi huo wa utafiti kwa Taifa ni upatikanaji wa takwimu sahihi wa madini ya kimkakati kwa ajili ya mamlaka za juu kufanya maamuzi ya uendelezaji .
“Tulikuwa na kikao cha siku tatu cha wataalam wa pande zote mbili cha kujadili ni kwa namna gani tutaendesha zoezi hili ,kazi kubwa tunatakiwakufanya utafiti wa kina” amesema Profesa Mtambo.
Profesa Mtambo amesema tafiti mbalimbali za awali zimenyika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambazo zimeonesha madini ya kimkakati yapo katika baadhi yavmaeneo hapa nchini.
Amesema ushiriano huo utahusisha kuwepo na timu ya Wataalam wa kufanya utafiti wa kina wa kuangalia madini yapo kwa kiasi gani , eneo gani, yanathamani gani na kwa viwanda vya aina gani .
Amesema baada ya utafiti huo wa kina kubainisha hayo ,tutaweza kuwekeza katika m
aeneo hayo ili iwe chachu kwa ajili ya kuanzisha viwanda vikubwa , vya kati, vidogo na vidogo zaidi ili kusaidia kuleta ajira nchini.
Profesa Mtambo amesema kuwa na andiko la mradi huo utawezesha upatikanaji wa fedha toka taasisi za kifedha kwa ajili ya utekelezaji na kuongeza chachu ya uendelezaji wa rasilimali za madini kwa ajili ya uchumi endelevu wa viwanda nchini .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO ,CPA Dk Venance Mwasse amesema kwa sasa wanatekeleza ajenda ya viwanda , na kwamba viwanda malighafi yake kuu ni madini.
Amesema ushirikiano na wenzao wa Tirdo ambao wanahusika na ufafiti na kutoa ushauri katika kuendeleza viwanda nchini, pia utekelezaji wa dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ambayo suala la Madini limeongelewa kwa kipaumbele kikubwa zaidi .
“ Dunia ya sasa ipo kwenye mageuzi ya nne na ya tano ya Viwanda , ambayo yanahitaji teknolojia ya malighafi na malighafi inachangiwa na madini ya kimkakati ambayo hapa nchini tunayo “ amesema