Pipi Jojo Sijamsign, Namsaidia kwa UpendoPipi Jojo Sijamsign, Namsaidia kwa Upendo

MENEJA wa Msanii wa Bongo Fleva, Grady Godlove ‘Pipi Jojo’, maarufu kama Chief Godlove, amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii huyo, akisisitiza kuwa hana mkataba rasmi naye bali anamsaidia kwa upendo na kama baba anavyomsaidia mwanae.

Akizungumza na Spoti Leo, Chief Godlove amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuuliza iwapo amemsainisha Pipi Jojo katika lebo yake ya muziki, lakini jibu lake ni hapana. “Mambo yote niliyofanya, nimefanya kama baba anavyomsapoti mwanae kufikia ndoto zake. Ni malezi ya baba kwa mwanae. Mawakili wangu hawajapitisha wino,” amesema.

Chief Godlove pia alifichua kuwa tayari amefungua lebo ya muziki kwa ajili ya kusapoti wasanii na kufanya biashara ya muziki kimataifa, lakini mpaka sasa hakuna msanii aliyesainiwa. “Ni kweli nimefungua label ya muziki kwa ajili ya kusapoti na kufanya biashara ya muziki internationally, siyo local. Uwekezaji upo, lakini Pipi bado hajasainiwa, na hadi sasa sijui ni nani atakuwa wa kwanza kusainiwa iwe Pipi au mwingine,” ameongeza.

Ameeleza masharti ya mkataba wa lebo hiyo endapo Pipi Jojo ataamua kusaini: “Kama Pipi Jojo atasaini kwenye label, basi asilimia 30 ya mapato yatakuwa yake, na asilimia 70 yatakuwa ya label kwa ajili ya kusimamia kila kitu kinachomhusu. Mkataba ni wa miaka 10,” amesema.

Chief Godlove amefichua kuwa tayari kuna video tano za Pipi Jojo ambazo bado hazijatolewa, akiwataka mashabiki kujiandaa kwa kazi bora zaidi kutoka kwa msanii huyo. SOMA: Wasanii waalikwa tamasha la muziki Morocco

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *