‘Mwigulu atayabeba maono Dira 2050’‘Mwigulu atayabeba maono Dira 2050’

WAZIRI Mkuu mteule, Dk Mwigulu Nchemba anatajwa kuwa ni mtu mwenye maono ya kujua taifa linataka kwenda wapi. Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema hayo bungeni Dodoma baada ya Dk Mwigulu kutangazwa kupendekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan awe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema sehemu ya maono hayo ni kuwa Dk Mwigulu atakuwa ni Waziri Mkuu anayelitazama taifa kwa miaka 25 mbele, kutokana na kuwa ni miongoni mwa mawaziri walioshiriki katika kuandaa Dira 2050, hivyo utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan unahitaji mtu wa aina yake.

Jenista amesema mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yaliyoelezwa yasingepatikana kama kusingekuwa na Waziri wa Fedha ambaye angetekeleza majukumu yake, ikiwemo kusaidia ongezeko akiwa ni miongoni mwa mawaziri ambao wametengeneza dira ya taifa ambayo tutakwenda nayo hadi 2050,” alisema Jenista.

Ameongeza kwamba, nchi inakwenda kupata Waziri Mkuu ambaye analitazama taifa hadi 2050, akisisitiza mbali na Dira 2050, Dk Mwigulu alikuwa ni miongoni wa wajumbe walioandaa Ilani ya Uchaguzi 2025/2030, hivyo anaifahamu ilani hiyo na atakwenda kuisimamia vizuri.

Katika hatua nyingine, Jenista alisema utekelezaji wa maoni ya Rais Samia kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM na yale ya ndani ya siku 100 za uongozi wake ambayo yanakwenda kumgusa Mtanzania mpaka wa hali ya chini, yanahitaji Waziri Mkuu kama Dk Mwigulu ili yaweze kutekelezeka.

Jenista amesema maono ya Rais Samia ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya, ujenzi wa Uchumi, mabadiliko ya kimfumo ndani ya serikali na usimamizi wa serikali yatakwenda kufanikiwa kwa sifa alizonazo Dk Mwigulu.

Amesisitiza wamepata chaguo sahihi na watakwenda kusimama naye na kutekeleza majukumu yao kama wabunge na kumsaidia rais na serikali kufikia malengo. SOMA:  Sifa za Dira ya Taifa 2050 zaelezwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *