Othman asisitiza wananchi kudumisha amaniOthman asisitiza wananchi kudumisha amani

ZANZIBAR: MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) Taifa, Othman Masoud Othman amewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea kudumisha amani ya nchi, licha ya chama hicho kupoteza ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

Alisema hayo wakati akihudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa, Micheweni Pemba na kuhudhuriwa na wananchi wa wilaya hiyo na maeneo ya jirani. Alisema subira ni kitu kikubwa ambapo waja wametakiwa kuwa nacho, ikiwemo kujiepusha na chuki na hasara ambazo madhara yake ni makubwa.

Othman alisema anafahamu wananchi wengi, wakiwemo wafuasi wa chama hicho wamehuzunishwa na matokeo hayo lakini wanatakiwa kumtanguliza Mungu, wakijua kila jambo hupangwa na Mungu na baadaye kulipa baraka zake.

“Najua wananchi wengi, wakiwemo wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo wamesikitishwa na matokeo ya Uchaguzi Mkuu ambapo chama chetu kimepoteza ushindi lakini nataka wavute subira na kufahamu kwamba, kila kitu kinafanyika kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,’’ alisema.

Kwa upande wake, Imamu wa msikiti huo, Shaame Mbwana Shaame aliwakumbusha waumini siku zote kufanya mambo mema ambayo humpendeza Mwenyezi Mungu na kujiepusha na chuki na kufanya uhasidi.

“Maamrisho ya Mwenyezi Mungu siku zote yanasisitiza waja wake kutenda mambo mema na kujiepusha na matukio ambayo yatamkera na kuwa chanzo cha kuwaingiza katika moto waja wake,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid alisema chama cha ACT Wazalendo kipo imara, licha ya kupoteza ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 ambapo kasoro za uchaguzi zilijitokeza. “Sisi viongozi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *