#HABARI: Mkutano wa Maaskofu Wakatoliki wa Marekani umelaani msako mkali uliotekelezwa na Idara ya Uhamiaji nchini ambao Rais wa Marekani Donald Trump anatetea kwa kile alichokiita “mageuzi ya msingi ya uhamiaji.””Tunasumbuliwa na vitisho dhidi ya utakatifu wa nyumba za ibada na hali maalum ya hospitali na shule,” maaskofu walisema katika ujumbe maalum, wa kwanza wa aina yake katika kipindi cha miaka 12.

Idara ya usalama wa ndani, ambayo inasimamia shughuli za uhamiaji, haikutoa maoni yoyote kuhusu hili. Ujumbe huo unarejelea ukosoaji kama huo uliotolewa na Papa Leo, ambaye ametoa wito wa “tafakari ya kina” kuhusu namna wahamiaji wanavyotendewa nchini Marekani chini ya utawala wa Trump.

Utawala wa Trump umeendeleza ajenda kali ya uhamiaji tangu alipoingia madarakani mapema mwaka huu.Trump amefuta sera ambayo inaweka kikomo cha kukamatwa kwa wahamiaji karibu na maeneo nyeti, ikiwa ni pamoja na makanisa, hospitali na shule, na kupeleka maafisa wa shirikisho kote Marekani ili kuimarisha zoezi la ukamataji huko.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *