Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa waasiwa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda pamoja na wanajeshi wa jeshi la Congo FARDC na makundi yenye silaha kama vile Wazalendo walitekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki mashariki mwa DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliotumwa kuchunguza hali katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini, umebaini katika ripoti yao kwamba pande zote kwenye mzozo wa mashariki wa DRC zilitekeleza ukatili tangu mwishoni mwa 2024.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna uwezekano kulifanyika uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, pande zote zikitajwa kuhusika katika mauaji ya kiholela, kutoweka kwa raia na ukatili wa kingono.

Waasi wa M23 huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 7 Aprili 2025.
Waasi wa M23 huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 7 Aprili 2025. REUTERS – Arlette Bashizi

Tangu kuzuka tena kwa mapigano mwishoni mwa 2021, waasi wa M23 wamedhibiti maeneo kadhaa mashariki mwa DRC kwa na kusababisha janga kubwa la kibinadamu.

Makabiliano mapya yalizuka mapema mwaka huu wakati waasi wa M23 walipouteka miji kadhaa ya Goma na Bukavu na kutangaza utawala mbadala katika maeneo hayo.

Wakati huu ukiukaji wa haki ukiendelea kuripotiwa, ripoti hiyo inasema ni lazima serikali za DRC na Rwanda zichukue hatua za haraka kuhakikisha sheria uy akimataifa inaheshimiwa na vikosi vyao na makundi yenye silaha washirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *