RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwnyi wiki hii anatarajiwa kuzindua uuzaji wa nyumba za Shirika la Nyumba Zanzibar zilizopo Kisakasaka, Wilaya ya Magharibi B kisiwani Unguja kwa ajili ya makazi ya wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Sultan Said Suleiman alisema nyumba hizo zipo katika makundi tofauti na zimejengwa kwa ajili ya wananchi wote.Suleiman amesema nyumba hizo zinaanza kwa gharama ya Sh milioni 92 na kuendelea mpaka Sh milioni 300 na muda wa kulipa ni miaka 25.

“Shirika tunajenga nyumba kubwa nzuri lakini ni rahisi kwenye ununuzi haina maana kuwa rahisi ni mbaya hapana tupo kwa ajili ya kuwapatia makazi mazuri wananchi,” alisema. Suleiman amesema licha ya kuzindua mauzo vilevile siku hiyo watazindua mwongozo wa shirika la nyumba kwa muda wa miaka mitano ijayo katika utekelezaji wa majukumu wa shirika hilo na mlolongo wa mauzo yatakavyofanyika.

Aidha, amesema  mpango wa serikali ni kuona inawasaidia wananchi kupata makazi hivyo mifumo ya ununuaji wa nyumba hizo utakuwa rahisi ili kumuwezesha kila mmoja kumiliki nyumba wakiwemo wafanyakazi wa serikali wanaoweza kununua nyumba kwa gharama kidogo.

Amesema  nyumba hizo zipo katika mgawanyo na ukubwa tofauti zikiwemo za vyumba vitatu, vinne na hata vyumba viwili kwa nyumba ndogo kwa kuwazingatia watu wanaoanza maisha. SOMA: Dk Mwinyi: Sitovumilia ugomvi wizarani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *