Polisi ya Tanzania iimetangza kuwa imemkamata raia wa Marekani na Kenya akiwa na mabomu katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya imesema: Mshukiwa huyo alikamatwa jana novemba 16 katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya la Sirali.

Taarifa hiyo imemtaja mshukiwa huyo kama Charles Onkuri Ongeta mwenye umri wa miaka 30 na kwamba ana uraia pacha wa Marekani na Kenya.

Charles Ongeta pia ametajwa kuwa ni mwanajeshi wa Jeshi la Marekani mwenye cheo cha Sajenti na kwamba amekamatwa akiwa na mabomu manne aina ya CS M68 ya kurusha kwa mkono akitokea Kenya kuingia Tanzania kwa kutumia gari aina ya Toyota Landcruiser.

Taarifa hiyo inasema: Mabomu hayo kwa mujibu wa Sheria ya Umiliki wa Silaha, hata kama angeomba kibali cha kuingia nayo nchini asingeruhusiwa.

Taarifa ya Polisi ya Tanzania imesema: Ushahidi unaendelea kukusanywa sambamba na kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki, kwa mujibu wa sheria, ziweze kuchukuliwa.

Tanzania ilishuhudia ghasia na machafuko makubwa wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29. Ripoti zinasema makumi ya watu walioawa katika ghasia na machafuko hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *