TANGA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman ametoa kiasi cha Sh milioni 13.4 kuwalipia madeni vijana waliokopeshwa na serikali mikopo ya asilimia 10.

Vijana hao 10 wa kikundi cha bodaboda cha Hatupoi walifanikiwa kupata mkopo wa Sh milioni 27.5 ambazo walinunua pikipiki nane na kufanikiwa kurejesha Sh milioni 14.1katika kipindi cha miezi nane.

Mwenyekiti huyo amevutiwa na urejeshwaji mzuri wa fedha za mkopo huo uliofanywa na vijana na hivyo kuamua kuwalipia mkopo wote uliobaki.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo Mwenyekiti wa CCM mkoa waTanga amewataka wanufaika wengine wa mikopo ya asilimia 10 kuiga mfano wa kikundi hivyo pale unapokopeshwa kulipa kwa wakati.

“Lengo la mikopo hii ndugu zangu ni kuhakikisha mnaitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kujiimarisha kiuchumi lakini na kufanya marejesho kwa wakati ili wengine waweze kunufaika,” amesema mwenyekiti huyo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Pangani Sekela amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 halmashauri hiyo imeweza kutoa mikopo ya Sh 304 kwa vikundi 48.

Akizungumza kikundi cha Hatupoi alisema kuwa kimemuwa ni mfano wa kuigwa kutokana na nidhamu yao ya urejeshaji kwa wakati wa fedha hizo za mikopo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha hatupoi Alhaji Kidau amesema kuwa walifanikiwa kupata mkopo wa sh Mil 27.5 ambazo walitumia kwa ajili ya kununua pikipiki nane za kufanya shughuli ya bodaboda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *