DODOMA; RAIS wa Tanzania,  Dk Samia Suluhu Hassan leo ametangaza Baraza jipya la Mawaziri lenye mawaziri 27 na Naibu Mawaziri 29.

Baadhi ya majina maarufu ambayo yalikuwepo kwenye Baraza la Mawaziri kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 29, 2025 ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Wengine ambao wanakosekana ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana, aliyekuwa Waziri wa Afya, Jenesta Mhagama, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jaffo.

Miongoni mwa sura mpya katika baraza hilo ni k Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Riziki Shemdoe kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza wakati akitangaza baraza hilo, Rais Samia amesema amehamisha majukumu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutoka Ofisi ya Rais badala yake yatakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo amemteua Prof. Riziki Shemdoe kuwa Waziri wa Tamisemi.

Sura nyingine mpya ni Daniel Chongolo aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo,  Joel Nanauka kuwa Waziri Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Judith Kapinga kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Dk Bashiru Ally Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *