
Jeshi la Israel limeharibu jengo jingine refu katika Jiji la Gaza siku ya Jumamosi, Septemba 6, likiwataka wakazi wake kuondoka kuelekea eneo ambalo limetangaza kuwa “la kibinadamu,” kwa kutarajia shambulio la ardhini baada ya miezi 23 ya vita. Umoja wa Mataifa unakadiria idadi ya watu katika eneo hilo kuwa karibu milioni 1 na kuonya juu ya “maafa” yanayokuja ikiwa hujuma ya Israel katika jiji hilo itapanuka.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Israel inaendelea na mashambulizi yake katika Mji wa Gaza, ambapo jeshi la Israel limeharibu jengo jingine refu katika huu siku ya Jumamosi, Septemba 6. Walioshuhudia wameliambia shiria la habari la AFP kwamba ni Mnara wa Soussi, ulio katika eneo la uhamishaji sawa na Mnara wa Ruya, ambao jeshi la Israel lilitangaza awali kukutaka kulenga. “Tunaendelea,” Waziri wa Ulinzi Israel Katz ameandika kwenye mtandao wa kijamii, akinukuu video iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha jengo hilo la ghorofa kumi na tano likiporomoka kwenye wingu kubwa la vumbi, anaripoti mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul.
Siku moja kabla, Ijumaa, Septemba 5, jeshi la Israel lilionya kwamba lingelenga “miundombinu ya kigaidi” katika Jiji la Gaza, hasa majengo ya juu. Jeshi la Israeli linashutumu Hamas, ambayo imetaja “uongo wa wazi,” kwa kutumia majengo haya kufanya operesheni zake.
Jeshi, ambalo linadai kudhibiti takriban 75% ya Ukanda wa Gaza na 40% ya Mji wa Gaza, linasema linataka kuwakamata ili kuwashinda Hamas na kuwaachilia mateka ambao bado wanawashikilia.
Mnamo mwezi Agosti Hamas ilikubali pendekezo la kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka lililowasilishwa na wapatanishi (Misri, Marekani na Qatar). Lakini serikali ya Benjamin Netanyahu inaitaka iweke silaha chini na inasema inataka kuchukua udhibiti wa usalama wa Ukanda wa Gaza.
Eneo la kibinadamu
Hapo awali, msemaji wa jeshi la Israel anayezungumza lugha ya Kiarabu alitoa wito kwa wakaazi wa mji huo kuhamia eneo jipya la kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, katika eneo la Khan Younis. Eneo ndogo la kilomita chache za mraba ambalo linapatikana katika eneo la Al Mawassi, ambalo, kulingana na jeshi la Israel, lina hospitali, maji, chakula na dawa.
Tangazo hili linapingana na ukweli uliopo. Wakazi wa Gaza, kama vile mtafiti Mustafa Ibrahim, aliyehojiwa na gazeti la kila siku la Haaretz, wanadai kwamba “hakuna hata mita moja ya mraba ya ardhi huru” katika ukanda huo. Wakazi wanaelezea hali mbaya ya msongamano wa watu huku kukiwa na uhasama unaoendelea.