Nchini Kenya kesi za muda mrefu za Paul Mackenzie zinaendelea, huku kesi zikisikizwa wiki hii katika mahakama ya watoto ya Tononoka mjini Mombasa, pwani ya Kenya. Mchungaji huyo na washitakiwa wenzake 35 wanashukiwa kuwafanyia ukatili na kuwatesa watoto kufuatia kupatikana kwa miili zaidi ya 450 mwaka 2023 katika msitu wa Shakahola, ambapo alihubiri kujizuia kula kabisa ili kuungana na Yesu. Ripoti ya ukaguzi wa simu zake za rununu uliwasilishwa kortini siku ya  Ijumaa, Septemba 5.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Inspekta Mkuu Joseph Kolum ameonya: “Uzito wa ushahidi uliotolewa na ripoti ya ukaguzi wa simu mbili za rununu za Paul Mackenzie ni mkubwa.”

Maelfu ya mazungumzo ya WhatsApp yamekusanywa katika hati ya karibu kurasa 76,000. Mahubiri ya Mchungaji Paul Mackenzie pia yanakusanywa katika hati za PDF, faili za sauti, na video.

Shuhuda kwenye simu zake nyingi zilikuwa ni za maneno “kufunga, unabii, Mpinga Kristo, Mnyama, utaratibu mpya wa ulimwengu, au nambari 666,” kama ilivyoichuliwa na mahakama.

Kuanzia mwaka wa 2020, Paul Mackenzie aliwasiliana na wafuasi wake wote kote nchini Kenya kuwaomba kuishi Shakahola. “Misheni yangu imekamilika,” aliandika, “lazima sasa tumngojee Bwana katika asili,” mkutano ambao ungeweza tu kufanyika kwa kujizuia kula kabisa, na kila mfuasi akikubalia kufaa kwa njaa ili “kuungana na Yesu.”

Ili kufikia malengo yake, mchungaji alitoa maagizo yaliyo wazi. Kwanza, kujitenge na jamii na kuwatoa watoto shuleni, kukataa matibabu, miongoni mwa mambo mengine. Kisha, kununua kiwanja katika msitu wa Shakahola na kufa katika eneo hilo.

Kati ya miili 450 iliyopatikana msituni, karibu nusu ni ya watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *