Camavinga

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya pauni £52.5m kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid raia wa Ufaransa Eduardo Camavinga, mwenye umri wa miaka 23. (Caughtoffside)

Everton hawatapokea ofa yoyote kwa winga wa Senegal Iliman Ndiaye, 25, na hawana nia ya kumuuza kwa mahasimu wao wa jiji, Liverpool. (Teamtalk)

Manchester City wanazingatia kulipa fungu la kuachiliwa cha £65m kilichopo kwenye mkataba wa mshambuliaji wa Bournemouth na raia wa Ghana Antoine Semenyo, 25, mwezi Januari. (Times)

Unaweza kusoma
Antoine Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Jurgen Klopp amejitolea kikamilifu kwa majukumu yake kama mkuu wa soka la kimataifa la Red Bull, na inaonekana hakuna uwezekano wa kurejea Liverpool endapo Arne Slot ataondoka Anfield. (Telegraph)

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Beta, anaongoza jitihada za klabu hiyo kumsajili kiungo wa kati wa Elche raia wa Hispania Rodrigo Mendoza, mwenye umri wa miaka 20, kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Chelsea na Tottenham wako tayari kupambana na Arsenal ili kumsajili Mendoza. (Teamtalk)

Mendoza

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wako makini katika jaribio lao la kumsajili kiungo wa Real Madrid raia wa Uruguay Federico Valverde, na watajaribu kutumia fursa endapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ataonesha nia yoyote ya kuhamia Old Trafford. (Fichajes)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, anasema mshambuliaji wa England na Manchester United anayekipiga kwa mkopo, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 28, ni “mwenye furaha” katika klabu hiyo na wanataka kumbakisha endapo itawezekana. (Times)

Manchester United wanatarajiwa kumkaribisha klabuni kiungo wa Colombia mwenye umri wa miaka 17 Cristian Orozco katika siku chache zijazo, huku uhamisho wake kutoka Fortaleza CEIF ukitarajiwa kukamilika mwezi Julai. (Daily Star)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *