MTWARA: Waziri wa Vijana, Joeli Nanauka amesisitiza kuwa umuhimu wa ushiriki wa sekta mbalimbali katika kukuza afya, umoja na maendeleo ya kijamii kupitia michezo.

Nanauka ambaye alikuwa mgeni rasmi wa msimu wa nne wa Korosho Marathon mkoani Mtwara alieleza umuhimu wadau kushiriki katika matukio hayo.

SOMA: Korosho Marathon yaja kwa watoto, wazee

Benki ya Exim ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio za Kilomita tano na kuonesha utayari wake kushiriki katika matukio hayo ya kijamii yenye lengo la kuboresha afya.

Mwakilishi wa Exim Bank katika tukio hilo aliahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kushiriki na kuunga mkono miradi inayogusa jamii kwani inaamini kuwa michezo ni jukwaa muhimu la kuhamasisha maendeleo chanya, kuimarisha mahusiano ya kijamii na kujenga taifa lenye afya bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *