Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, imefanya Bonanza la Michezo la Watumishi lengo likiwa kuendelea kuhamasisha amani ndani ya Halmashauri hiyo na Tanzania kwa Ujumla.
Katika Bonanza hilo ambalo lilihusisha watumishi wa Tarafa zote tano za Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mgeni Rasmi, alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Ikupa Harrison Mwasyoge.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo, Dkt. Mwasyoge alisema kwamba kupitia Bonanza Hilo watumishi hususani Vijana wanaweza kupata fursa ya kujadiliana mambo yao na kujadiliana fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia..
Lakini pia alisema maandalizi ya bonanza Hilo yamefanikiwa kwa sababu Kuna amani nchini hivyo watumishi wanatakiwa kuendelea kubeba ujumbe wa amani kila waendapo.
Katika hatua nyingine, Bonanza Hilo lilitumika kutoa elimu mbalimbali za masuala ya maambikizi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na kupima, Elimu hiyo ilitolewa na Mratibu wa Ukimwi Lushoto, Esuvat Kivuyo.
(Feed generated with FetchRSS)