Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua waziri wake wa ulinzi na mshirika wake wa karibu Sebastien Lecornu kama waziri mkuu mpya ili kutatua mzozo wa kisiasa unaozidi kuongezeka huku maandamano yakikaribia kufanyika siku zijazo.

Macron alimchagua Lecornu, 39, hapo jana kuchukua nafasi ya Francois Bayrou kama waziri mkuu wa saba wa mamlaka yake, akimpigia debe mmoja wa washirika wake wa karibu badala ya kutaka kutanua kukubalika kwa serikali katika wigo wa kisiasa.

Ofisi ya rais imetangaza kwamba Macron amemtaka Lecornu ashauriane na makundi ya kisiasa yanayowakilishwa bungeni kwa nia ya kupitisha bajeti ya taifa na kufanya makubaliano kuwa muhimu kwa maamuzi ya miezi ijayo. 

Kwa kujibu, Lecornu alimshukuru Macron kwa imani yake, na akamsifu Bayrou “kwa ujasiri alioonyesha katika kutetea imani yake hadi mwisho.

Makabidhiano rasmi ya mamlaka kati ya Bayrou na Lecornu yanatarajiwa kufanyika leo saa sita mchana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *