Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amemtua Waziri wake wa Ulinzi Sebastien Lecornu, kuwa Waziri wake Mkuu, baada ya bunge kupiga kura ya kukosa imani na mtangulizi wake François Bayrou.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Lecornu, anakuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Ufaransa, katika kipindi cha mwaka mmoja, wakati huu uongozi wa Macron ukiendelea kujipata katika sintofahamu ya kisiasa, kutokana na mvutano kuhusu bajeti ya taifa na mpango wa kubana matumizi.
Waziri Mkuu huyu mpya, anaingia Ofisini siku ya Jumatano, wakati maandamano makubwa yakipangwa na wafanayakazi wa sekta ya uchukuzi na elimu kuonesha hasira dhidi ya uongozi wa Macron.

Hatua hii inatarajiwa kuwa changamoto kubwa kwa Lecornu, mwenye umri wa miaka 39, mshirika wa karibu wa Macron ambaye kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, amekuwa Waziri wa Ulinzi.
Aidha, haijafahamika vema mpango wa Lecornu kuhusu suala la upitishwaji wa bajeti bungeni na namna atakavyopambana na deni la taifa linaloendelea kuongezeka.