Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) wametia saini makubaliano mjini Cairo siku ya Jumanne, Septemba 9, na kufungua njia ya kuanza tena ushirikiano, ikiwa ni pamoja na njia za kuanza tena ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Iran na IAEA zimefikia maelewano kuhusu jinsi ya kuchukua hatua katika muktadha huu mpya,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghai amesema kwenye televisheni ya taifa. Tangazo hili lilifuatia mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty, mwenzake wa Iran Abbas Araghchi, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Rafael Grossi.

Wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Badr Abdelatty ameelezea matumaini yake kwamba makubaliano hayo yanaweza “kukuza maelewano” kwanza na nchi za Ulaya ambazo zilitishia kurejesha vikwazo, na kisha “kusababisha kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani.” Rafael Grossi, kwa upande wake, amepongeza kama “hatua muhimu katika mwelekeo sahihi.” Ameonyesha kuwa amekubaliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran “juu ya mbinu za kivitendo za kuanza tena ukaguzi nchini Iran” wa shughuli za nyuklia.

Vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza

Mkutano huo unakuja katika wakati nyeti, huku Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zikianza mchakato wa kuiwekea tena vikwazo Iran mnamo Agosti 28 kwa kile wanachokiona kuwa ni kushindwa kufuata makubaliano ya mwaka 2015 yaliyolenga kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Tarehe 2 Julai, Rais wa Iran Massoud Pezeshkian alitia saini sheria iliyopitishwa na bunge la nchi yake ya kusitisha ushirikiano wote na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA). Sheria hii inafuatia vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran mwezi Juni, ambapo Israel na Marekani zilishambulia maeneo ya nyuklia ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *