
Haya yamesemwa na maafisa nchini humo Alhamis huku watu watano wengine wakiwa hawajulikani walipo.
Katika taarifa, msemaji wa Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na MajangaIndonesia Abdul Muhari, amesema zaidi ya watu 500 wameokolewa huku shule, misikiti na kumbi za vijijini vikigeuzwa kuwa hifadhi za muda.
Mvua kubwa iliyonyesha Bali kuanzia jioni ya Jumanne ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika wilaya saba.
Hali ya hewa katika mji mkuu wa mkoa wa Bali, Denpasar, ni nzuri kwa sasa ingawa shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia linasema huenda kukashuhudiwa ya kadri katika mikoa kadhaa ukiwemo mkoa wa Bali kesho Ijumaa na Jumatatu.