Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM.

Shirika hilo limetoa wito wa karibu dola milioni 17 ili kuwapa makaazi na huduma za afya za dharura waathirika zaidi ya laki moja wa tetemeko hilo la ardhi.

Kulingana na naibu mkurugenzi mkuu wa IOM Ugochi Daniels, familia zimepoteza kila walichokuwa nacho na sasa zinalala nje.

Tetemeko hilo la ardhi liliipiga Afghanistan usiku wa kuamkia Septemba mosi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 na kuharibu zaidi ya nyumba elfu saba. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema zaidi ya watu nusu milioni waliathirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *