Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa, Septemba 12, katika kesi ambayo Joseph Kabila hajahudhuria. Akituhumiwa kushirikiana na kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, rais huyo wa zamani, ambaye amekuwa akiishi uhamishoni kwa zaidi ya miaka miwili, anashitakiwa na Mahakama Kuu ya Kijeshi na anakabiliwa na hukumu ya kifo.
