Serikali nchini Nigeria, imewafukuza nchini humo wageni 102 wakiwemo raia wa China 50, waliopatikana na makosa ya uhalifu wa mtandaoni na udanganyifu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria, imethibitisha hatua hii, ikisema raia mmoja wa Tunisia ni miongoni mwa wageni hao waliorudishwa katika nchi zao, tangu Agosti tarehe 15.

Aidha, Tume hiyo imesema inapanga kuwaondoa nchini humo, wageni zaidi baada ya kuwakamata 792, wakiwemo wenyeji waliokuwa wanajishughulisha na uhalifu wa mtandaoni kwenye kisiwa cha Victoria, jijini Lagos, mwezi Desemba mwaka uliopita.

Miongoni mwa waliotiwa mbaroni ni raia wa kigeni 192, ambapo Wachina walikuwa ni 148.

Taifa hilo la Afrika Magharibi lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, kwa muda mrefu, limekuwa na sifa mbaya ya kuongoza kwenye uhalifu wa mtandao kwa kuwatapeli watu, kutumia wahalifu waliopewa jina la “Yahoo Boys”.

Wanaolengwa kwenye uhalifu huo, kwa lengo la kujipatia fedha, ni Wamarekani, raia kutoka Canada, Mexico na watu kutoka mataifa ya Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *