Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, ameshtakiwa kwa “ugaidi na uhaini,” Wizara ya Sheria ya Sudan Kusini imetangaza katika taarifa yake siku ya Alhamisi, Septemba 11. Riek Machar, mwanasiasa wa upinzani na mpinzani wa milele wa Rais Salva Kiir, yuko chini ya kizuizi cha nyumbani kwa miezi sita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, anashtakiwa kwa “mauaji, ugaidi, uhaini na uhalifu dhidi ya ubinadamu.” Kulingana na taarifa ya Wizara ya Sheria, anashukiwa kuwa na hatia ya kuratibu, pamoja na washitakiwa wenzake saba, shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwezi Machi. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya “zaidi ya wanajeshi 250,” pamoja na meja jenerali wa Sudan Kusini na rubani wa Umoja wa Mataifa. Riek Machar alikamatwa baadaye na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.

Ushindani kati ya Rais Salva Kiir na makamu wake umeendelea kutia sumu katika anga ya kisiasa nchini Sudan Kusini. Baada tu ya kupata uhuru, nchi hiyo ilitumbukia katika miaka minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Chini ya shinikizo la kimataifa, wawili hao walikubali kugawana madaraka katika serikali ya mpito. Lakini tangu wakati huo, uhusiano wao umeendelea kuzorota. Mvutano ulifikia kilele mapema mwaka huu kutokana na mapigano ya silaha kati ya wafuasi wa watu hao wawili katika mikoa kadhaa ya nchi na mfululizo wa kukamatwa kwa washirika wa karibu wa Riek Machar. Mashitaka dhidi ya Riek Machar yanazua hofu, kwa mara nyingine tena, ya kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *