Nchini Côte d’Ivoire, siku moja baada ya kukataliwa kugombea urais, rais wa zamani Laurent Gbagbo amepokea wapinzani wengine kadhaa mnamo Septemba 10, 2025. Miongoni mwao ni Pascal Affi N’Guessan wa chama cha FPI.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Mkutano huo ulifanyika kwa faragha, katika ofisi ya rais wa zamani wa Côte d’Ivoire huko Cocody.

Laurent Gbagbo alimpokea Waziri Mkuu wake wa zamani (2000-2003), Pascal Affi N’Guessan, ambaye haelewani naye. “Tuko kwenye meli moja,” Pascal Affi N’Guessan amesema, akihalalisha mkutano huo.

Kwa hakika, ugombea wa rais wa Chama cha FPI pia ulionekana kuwa haukubaliki, kwani Baraza la Katiba lilibaini kwamba alikosa watu 20,000 wa kumuunga mkono.

“Kuanzisha mawasiliano”

Laurent Gbagbo kisha alikutana na uongozi wa chama cha PDCI-RDA, kilichowakilishwa haswa na Noel Akossi Bendjo, makamu wa rais wa PDCI-RDA.

Mkuu huyo wa zamani wa nchi hatimaye alizungumza na kiongozi wa vuguvugu la Guillaume Soro la Generations and Peoples in Solidarity (GPS), ambaye anaishi uhamishoni.

“Ilikuwa ni mkutano wa awali ili kupata mawasiliano,” alisema mmoja wa washiriki, ambaye hakufichua yaliyomo kwenye majadiliano.

Mikutano mingine ya aina hii inatarajiwa kuratibiwa tena.

Wakati huo huo, wanaharakati katika chama cha Laurent Gbagbo cha African People’s Party – Côte d’Ivoire (PPA-CI) wanaendelea kuunga mkono ugombea wa kiongozi wao. “Tutaendeleza mapambano ya amani ya kisiasa dhidi ya muhula wa nne [kwa Rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara] na kufanya kila tuwezalo kuhakikisha haki zetu zinaheshimiwa,” Sébastien Dano Djédjé, kiongozi mtendaji wa PPA-CI, alisema siku ya Jumanne jioni wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *