
Barua pepe zilizovuja zinaonesha kuwa Balozi Peter Mandelson alikuwa akiwasiliana na kumuunga mkono Epstein, akimueleza kuwa hukumu dhidi yake ilikuwa batili na kwamba lazima ipingwe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Stephen Doughty, aliliambia bunge hapo jana kwamba barua hizo zinaonesha kiwango cha juu cha mahusiano kati ya balozi huyo na Epstein, tafauti na taarifa ambazo mamlaka ilikuwa nazo wakati Mandelson akichunguzwa kabla ya uteuzi.
Suala la nyaraka za Epstein ni sehemu muhimu ya mjadala unaoendelea ndani ya Marekani, hasa baada ya uvumi kwamba Rais Trump mwenyewe alikuwa na mahusiano ya kina na mtuhumiwa huyo aliyefariki dunia akiwa jela mwaka 2019.