Waziri Mkuu wa Ufaransa mbioni kuunda serikali mpya
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu anafanya majadiliano ya kuunda serikali baada ya chama chake kumpoteza mshirika wake mkuu wa kisiasa.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu anafanya majadiliano ya kuunda serikali baada ya chama chake kumpoteza mshirika wake mkuu wa kisiasa.
Herminie anawakilisha chama cha United Seychelles, ambacho kiliongoza nchi hiyo kwa miongo minne kabla ya kupoteza mamlaka mwaka wa 2020. Kilikuwa chama tawala kutoka 1977 hadi 2020.
Ndege iliyobeba timu ya Nigeria kutoka Afrika Kusini kuelekea Uyo kwa mechi yao ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe la Dunia ililazimika kutua kwa dharura nchini Angola siku ya Jumamosi.
Kikosi cha wanajeshi waasi kimetangaza kuwa kinadhibiti vikosi vyote vya kijeshi vya Madagascar, huku Rais Andry Rajoelina akisema "jaribio la kunyakua mamlaka kinyume cha sheria" linaendelea nchini humo.
Mkutano wa kilele kuhusu amani ya Gaza utafanyika siku ya Jumatatu kwenye mji wa pwani wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
China imeishutumu Marekani kwa undumilakuwili baada ya Rais Donald Trump kutangaza ushuru wa ziada wa hadi asilimia 100 kuzitoza bidhaa za China zinazoingia Marekani.
Wananchi wa Cameroon wamepiga kura Jumapili (12.20.2025) katika uchaguzi mkuu utakaoamua hatma ya Rais Paul Biya mwenye miaka 92.
Mamlaka nchini Mexico imesema watu wapatao 41 wamekufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi kwenye eneo la kusini mashariki la nchi hiyo.
Mataifa ya Ulaya Jumapili (12,10.2025) yameanzisha mfumo mpya wa Kuingia na Kutoka kwa wasafiri ambao sio raia wa Ulaya.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani kitendo alichokiita ni cha uchokozi kutoka kwa nchi jirani ya Afghanistan.