Mamilioni ya watoto katika nchi nne za Afrika wanaweza kufa kwa utapiamlo katika muda wa miezi mitatu ijayo, mahitaji ya dharura ya chakula yakipungua kutokana na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa, limeonya shirika la Save the Children.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake Save the Children, imesema nchi za Nigeria, Kenya, Somalia na Sudan Kusini zilitarajiwa kukosa kile kinachoitwa “chakula cha matibabu kilicho tayari kutumika”, unga wa lishe ambao una maisha marefu na hauhitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu.

Shirika hilo linasema nchi ya Nigeria peke ake, maisha ya watoto milioni 3.5 walio chini ya umri wa miaka 5 ambao wanakabiliwa na utapiamlo yatakuwa kwenye tishio ikiwa hawatapata matibabu na msaada wa lishe.

Onyo hilo linakuja miezi michache kupita tangu Umoja wa Mataifa utangaze kupunguzwa kwa programu za chakula kwa kile ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu ilisema “kupungua kwa michango ya nchi wafadhili”.

Wafadhili wakuu wa kimataifa, wakiongozwa na Marekani, wamepunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa  kutoka nje, hatua iliyosababisha hofu na athari kubwa kwa mataifa ambayo yalikuwa yanategemea misaada kwa kiasi kikubwa.

Mwezi uliopita, shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF liliripoti kuwa angalau watoto 652 walio na utapiamlo walikufa katika vituo vyake kaskazini mwa Nigeria katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *