Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, limesema kuwa robo milioni ya watu wamesajiliwa kama waliopotea, idadi ambayo ni sawa na asilimia 70 katika kipindi cha miaka mitano, ripoti ya shirika hilo imeonesha.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ongezeko hili limechangiwa na idadi ya mizozo, watu kukimbia nchi zao na kuporomoka kwa utawala wa sheria kwenye mataifa mengi duniani.

Mkurugenzi wa ICRC, Pierre Krahenbuhi, amesema kuanzia Sudan, Ukraine, Syria hadi Colombia, tatizo liko wazi, ongezeko la watu wanaopotea likituma ujumbe kuwa pande hasimu na wale wanaowaunga mkono wameshindwa kuwalinda raia kwenye maeneo ya vita.

Ripoti imeongeza kuwa, mwaka 2024 watu zaidi ya laki 2 na elfu 84 waliripotiwa kupotea, huku kidunia mamilioni ya watu wakitenganishwa na familia zao kwa miaka hata miongo kadhaa.

ICRC inasisitiza kuwa mataifa na pande zinazohusika katika mizozo zinabeba jukumu la msingi la kuzuia watu kutoweka, kueleza hatima ya watu waliopotea na kutoa msaada kwa familia zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *