#HABARI: Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya Jumapili, ambapo atazungumza kuhusu sera na mikakati yake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleza maandalizi ya mkutano wa kampeni utakaofanyika Agosti 31, mwaka huu katika Viwanja vya Medeli jijini Dodoma.
Amesema maandalizi yote yamekamilika na wananchi wanatarajiwa kupata nafasi ya kusikiliza moja kwa moja sera za mgombea huyo, ambazo zinaelekeza muelekeo wa maendeleo ya taifa kwa miaka ijayo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania